Licha
ya kupigwa vita Msanii Diamond Platnum amezidi kuisafisha Nyota yake
ya Muziki kwa kuanza kuliangaikia soko la Kimataifa na kuhakikisha
anafanya vyema
kama ambavyo ameweza kufanikiwa kulishika soko la
ndani na kusimama katika nafasi za juu kabisaa za wasanii wa ndani
ambao wanaongoza kulipwa Pesa nyingi katika Shows.
Diamond
Platnum kwa sasa yupo nchini Nigeria akifanya Video ya wimbo wake wa
My Number 1 (Remix) ambao amemshirikisa Mkali Davido kutoka Nchini
Nigeria.
Akiwa
Nchini Nigeria Diamond aliweza kuhudhuria Sherehe za Ndoa ya Kimila
ya Peter wa Psquare na kupata nafasi ya kukutana na wakali wengine
kibao wa Nigeria akiwemo Emmanuel Adebayo,Iyanya na wengine wengi.









0 comments:
Post a Comment