Mkali wa My
Number 1 Diamond Platnum alikutana na waandishi wa gazeti la Michezo
la MwanaSpoti
alihojiwa mambo mengi kuhusu maisha yake
kabla na baada ya kuwa
Maarufu. Hii ni sehemu ya Interview aliyofanya na gazeti la
Mwanaspoti.
Diamond:
Nimewahi kuwa na wapenzi wanne katika kipindi chote cha
ustaa wangu na sikupenda kubadili ovyo ila wengi wao hawakuweza
kutimiza haja ya moyo wangu.
Mwanaspoti:
Unaweza
kuwataja majina?
Diamond:
Ndiyo ila wawili wanafahamika zaidi.
Wa kwanza kabisa
alikuwa anaitwa Sarah na wa pili alikuwa anaitwa Hawa yule msichana
niliyeimba naye katika wimbo ‘Nitarejea’, huyu alizidiwa ujanja
na Wema Sepetu ambaye naye alikuja kuondoka kwangu na baadaye nikawa
na Penieli Mungilwa.
Mwanaspoti:
Mwanamke
yupi unahisi ulimpenda kuliko wote?
Diamond:
Mwanamke
wangu wa kwanza Sarah Sadick huyu aliniingia sana moyoni sijajua ni
kwanini.
Lakini nahisi huenda
kwa kuwa awali alinipenda kweli kwa kuwa wakati huo sikuwa na kitu.
Hata hivyo nahisi
ilitokana na mimi kutokuwa bize na wakati huo sikufikiria lolote
zaidi ya yeye ilitokana na kutokuwa na kazi ya kufanya.
Siku hizi sina mapenzi
ya kivilee, nawaza zaidi pesa na ninaihangaikia na zaidi ni muziki
wangu, hili ndilo la kwanza kabisa linalonifanya niwe bize mapenzi
baadaye.







0 comments:
Post a Comment