Tuesday, November 26, 2013

BELLE9 KURUDI KIAFRIKA ZAIDI “WANANITAKA”

Baada ya kimya cha muda mrefu kutoka kwa Msanii Belle 9 ambaye ametamba na Hits Song kibao leo November 26 anadondosha ngoma yake inayokwenda kwa
jina la Wananitaka ambayo imebeba ujumbe wa Mapenzi lakini ikiwa na mahadhi ya Kiafrika Zaidi yenye kuburudisha na kuelimisha.

Belle 9 amefunguka kuwa ngoma yake hiyo ameifanya chini ya Maproduza Mawili Producer wake aliyemtoa ‘Tris’ ambaye hivi sasa yuko Afrika kusini ndiye aliyegonga Beat na Ngoma kaimalizia vocal kwa producer Mona Gangster.

Hiyo ngoma ni muziki flani hivi wa kiafrika kwa sababu sasa hivi African Music ndio muziki ambao umeiteka dunia nzima hata wasanii wa Afrika wanauza sana huko Ulaya. Watu wamezoea kunisikia sana kwenye beat za R&B sana, kwa hiyo round hii nimechange kidogo ili kutengeneza mazingira ya hata kupata nafasi sehemu za mbali.”

0 comments:

Post a Comment