Msanii wa Bongo Movie
ambae kwa sasa anafanya poa kunako fani ya utangazaji kwa kuwa na
kipindi cha Luninga kinachojishughulisha na kusaidia jamii
hususani
watu wenye mahitaji ya kuboresha nyumba zao ambazo zipo katika hali
mbaya kimuonekano na zinazoweza kusababisha hata hatari kwa wakazi wa
nyumba hizo.
Mwanadada Irene
ametangaza rasmi kuachana na kazi yake ya awali ambayo kwa namna moja
au nyingine ndiyo iliyomsaidia kupata mafanikio mbalimbali aliyonayo
sasa ikiwemo kupata mume ambae amezaa naye mtoto mmoja ingawa
inasemekana kuwa wawili hao walishakwisha tengana na kila mmoja
anaendelea na maisha yake.
Sababu kubwa za Irene
kuachana na kazi hiyo ni kutaka kutumia muda wake vizuri kushughulika
na kipindi chake cha luninga maana kama atafanya kazi zote mbili
inaweza kupunguza ufanisi wake katika kazi hizo ingawa aliongeza kuwa
ameamua pia kuwaachia watu wengine ambao hawajapata nafasi na wenye
malengo ya kuendelea na tasnia ya Bongo Movie kufanya kazi hiyo.
“Nimeamua kuacha
mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama
miezi sita iliyopita… Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita
iliyopita ”






0 comments:
Post a Comment