Tuesday, October 8, 2013

SIMBA WAMENIUMIZA SANA ILA DAWA YAO NINAYO-MRISHO NGASA

Winga Mrisho Ngasa wa Yanga amesema atacheza kwa nguvu zake na akili zake zote ili kuipa timu yake ya Yanga Ubingwa wa Ligi kuu Tanzania.

Baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara walioshinda 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi, Ngasa alisema ameumia sana sana kuilipa fedha Simba hivyo atafurahi kuona amelipa kisasi kwa kuifunga timu hiyo na kuiwezesha Timu yake kuwa Kileleni katika Msimamo wa Ligi.

"Imeniuma kupigwa faini kubwa wakati klabu ya (Simba) niliitumikia kwa nguvu zangu zote msimu uliopita. Kikubwa kwangu kwa sasa ni kucheza kwa kujituma zaidi ili Yanga ipate ubingwa msimu huu. Naamini kwa kufanya hivyo, nitakuwa nimewajibu Simba,"

0 comments:

Post a Comment