Tuesday, October 8, 2013

RAIS JK AMEPOTOSHWA KWA MAKUSUDI NA WALIOMPOTOSHA NI HAWA HAPA-MBOWE


Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amedai kuwa Rais Jakaya Kikwete amepotoshwa na baadhi ya
Viongozi wake kuwa mjadala wa bunge ulikwenda vizuri,Mbowe aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa siku nne wa wataalam mbalimbali wa Chadema kutoka kanda za kichama.

Kwa mujibu wa Freeman Mbowe mjadala wa Bunge haukwenda vizuri na hata wabunge wa CCM hawakuweza kujadili .


baada ya wabunge wa upinzani kuomba mwongozo na kunyimwa fursa hiyo hadi wakaamua kutoka nje, wabunge wa CCM waliobaki ndani hawakujadili muswada badala yake walirusha vijembe na kejeli kwa kambi ya upinzani.

“Kwa hiyo Rais anaposema mjadala wa Bunge ulikwenda vizuri ajue kwamba amepotoshwa kwa makusudi. Watu waliomweleza rais taarifa hizi ni akina Lukuvi (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge) na Wasira (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu), ambao walikuwa wanaturushia vijembe bungeni, Rais asome hansadi aone kilichojadiliwa,” .

0 comments:

Post a Comment