Friday, October 18, 2013

LINEX AFUATA NYAYO ZA DIAMOND,OMMY DIMPOZI NA AY.

Mkali wa Sauti ambaye alianza kuvuma kwa Mama Halima na kufanikiwa kupenya katika Masikio ya watanzania walio wengi na kuweza kukubalika kwa kazi zake
alizoendelea kuzidondosha Linex Sunday Mjeda kesho atakuwa akitambulisha video ya Wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la KIMUGINA.

LINEX ameomba watanzania waweze msupport kwa kuibuka katika Ukumbi wa Ambassador Lounge kwa kiingilio cha Elfu Kumi tu huku ukiweza kupata Burudani kutoka Kwa Linex Mwenyewe ambaye atasindikizwa na wakali kama Barnaba &Amini,Recho Stara Thomas pamoja Chidy BENZI.

Kwa wasanii wa Nyumbani kwa sasa wengi wameanza kuziona fursa za kutengenezea kipato kwa njia mbalimbali,wapo wasanii walioanza kuziona Fursa hizo mapema akiwemo Ladyjaydee,Ay na FA,Diamond Platnum pamoja na Ommy Dimpozi ambao nao wakiweza kuzindua video za kwa kufanya Party.

0 comments:

Post a Comment