Thursday, October 10, 2013

HIKI NDICHO P SQUARE WATAFANYA TANZANIA MWEZI UJAO.


Wakali kutoka Nigeria ambao watatua Tz na kufanya Show siku ya Tarehe 23 Mwezi Ujao nawazungumzia Peter na Paul ambao kwa pamoja wanaunda kundi la
PSQUARE wamepanga kufanya LIVE BAND itakayofanywa ndani ya masaa mawili bila kupumzika.

Mbali na kufanya hiyo show Live wakali hao watadondoka na Wasanii wengine 13 kufanya kazi hiyo ndani ya Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Dar es Salaam Muwakilishi wa East Africa Radio na Televison Hillary Daudi alimaarufu kama Zembwela amefunguka na kusema kuwa Sababu kubwa kuwaleta wasanii hao Tanzania ni kutoa fursa kwa watanzania kupata Burudani lakini pia Kuwapa shule wasanii wa Nyumbani Tanzania kuiga kile kizuri ambacho wale jamaa hukifanya.

0 comments:

Post a Comment