Wema Sepetu ni kati ya
Wasanii wachache Nchini wanaoongozwa kwa kuuza vichwa vya habari na
kusababisha biashara ya magazeti kuwa juu pindi tu anapotokea katika
Gazeti hilo kwa stori.
Mbali na kuongoza kwa
kuuza kwa magazeti kwa stori ambazo muda mwingine hupikwa na
waandishi kwa lengo la kufanya biashara na muda mwingine zikiwa na
uhalisia,pia Wema Sepetu anaongoza kwa kuandikwa katika vyombo vya
habari kwa skendo mbalimbali.
Kwa mujibu wa Wema
amedai kuwa kuka kimya kwake kwa mambo anayofanyiwa na waandishi hao
si kama yeye ni mjinga na wao kuchukua nafasi hiyo kuendelea
kumchafua pasipo na sababu,ametililika kuwa wamekuwa wakimzushia
mambo mengi sana na yeye kama binadamu yanamuumiza na kumtesa pia
lakini huwa anamua kupotezea tu.
Siku za karibuni
mwanadada huyo alielekea Nchini China na safari yake ya china
waandishi wengi waliihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na moja
ya gazeti pendwa liliibuka na kichwa cha Habari kisemacho WEMA
KUNYONGWA CHINA huku likipambwa na kichwa kidogo kisemacho AOMBA
WATANZANIA KUMUOMBEA huku kukiwa na Picha ya dawa za kulevya chini
yake kutokana na suala hilo ndipo mwanadada alipofunguka na kusema
kuwa anachukizwa sana na waandishi wa magazeti .
“I jus hate
waandishi wa habari wa ya mageziti ya bongo.. hususan visa nd filamu”







0 comments:
Post a Comment