Tuesday, October 1, 2013

MAJANGA MENGINE KWA GAZETI LA MWANANCHI NA RAI

Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupita kwa msemaji wa Serikali Assa Mwambene wamelipiga marufuku  gazeti la RAI kutoka kila siku na pia gazeti la MWANANCHI kutowekwa mtandaoni (online) hadi adhabu itapoisha.
Kwa Gazeti la Rai mwanzo lilikuwa likitoka kwa week mara moja lakini baada ya kufungiwa kwa Gazeti la Mwananchi RAI walianza kuchapisha Gazeti lao kila siku hivyo serikali imelitaka kurudia utaratibu wake wa awali wa kuchapisha gazeti hilo kila week na si kila siku.
na Upande wa MWANANCHI Kabla hata ya kufungiwa walikuwa na Website yao ambayo walikuwa wakiitumia kuweka Habari za Gazeti hilo hivyo hata baada ya kufungiwa waliendelea kuweka Habari zao kupitia mtandao huo hivyo serikali imewataka kutokuweka Habari hizo katika Mtandao wao,mpaka hapo adhabu yao itakapokwisha.



0 comments:

Post a Comment