Wednesday, October 23, 2013

DOGO NJANJA-SIJAFUKUZWA NIMEONDOKA MWENYEWE

Kwa mujibu wa Mitandao ya kijamii mbalimbali ilitoa taarifa kuwa msanii Dogo Janjalo ambaye kwa mara ya kwanza alikuwa chini ya Msanii Madee
kutoka TIP TOP COONECTION na uongozi mzima wa Tip Top ambapo kuwa ametimuliwa katika kundi linalo ongozwa na Ostaz Juma na Musoma.
Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa yeye hajatimuliwa bali ameamua mwenyewe kuondoka Watanashati na kwenda kujitegemea kama wasanii wengine ambao hawapo katika Uongozi wa mtu7 yoyote yule,Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye amekuwa mtu mzima hivyo hawezi kusihi kwa kupelekeshwa bali anaishi kwa kile anachoamuwa.
"Najua yatasemwa mengi kutoka kwa Ostaz Juma ila mimi ndio uwamuzi wangu, kuna watu wanasema sina utovu wa nidhamu lakini hao watakuwa wananijua sasa hivi hawajanifuatilia kutoka nyuma.

Hata mtoto mdogo atakuwa mtundu ila akiwa mkubwa hunyooka na kuwa mtoto mzuri sasa nimekuwa mkubwa na kupelekwa pelekwa tena sitaki, kwa maelezo zaidi Ostaz Juma aongee na wazazi wangu asiongee na mimi"(quotation source:Dj Choka)

Dogo Janja kabla ya kujiunga Watanashati alikuwa chini ya Msanii Madee ambaye ndiye alimtambulisha kwa jamii na baadaye walishindana na kuelekea Katika Kundi La Mtanashati akiwa chini ya Kiongozi Ostaz Juma na Musoma.

0 comments:

Post a Comment