Thursday, September 12, 2013

YANGA YATUA MBEYA BILA 'HARUNA NIYONZIMA'

Timu ya Yanga Jana iliwasili Jijini Mbeya kwa maandalizi ya kuzisaka point sita muhimu lakini mpaka wanawasili jijini Mbeya Kikosi cha Yanga kilikuwa hakina Mshambuliaji ambae ni tegemeo Mnyarwanda Haruna Niyonzima 'Fabregas'.
Yanga mpaka sasa ina pointi nne baada ya kucheza mechi mbili, Jumamosi itashuka kwenye Uwanja wa Sokoine kucheza dhidi ya Mbeya City kabla ya kucheza tena Jumatano kwenye uwanja huo dhidi ya 'maafande' Prisons.

Kwa mujibu wa Taarifa zilizopo zinadai kuwa Niyonzima alitarajiwa kuwasili jana Nchini akitokea Nchini Rwanda alipokwenda kuwakilisha Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi).lakini mpaka sasa hakuna taarifa zozote zilizotolewa na uongozi juu ya kuchelewa kwa Mshambuliaji huyo.

Kwa mujibu wa Historia, Niyonzima siyo mchezaji wa kwanza wa kimataifa kuchelewa kurejea katika klabu yake nchini baada ya kuruhusiwa kwenda kwao kwa muda kwa sababu mbalimbali ikiwamo ya kwenda kuzichezea timu zao za taifa.



0 comments:

Post a Comment