Thursday, September 12, 2013

SI LAZIMA KUFANYA WIMBO NA STAA TU-BEN PAUL

Mkali wa muziki wa RnB Tanzania anaendelea kufanya poa na ngoma yake ya JIKUBALI ambayo ilifanywa na Produza Lucci...!
Ben PAUL Amefunguka na kusema kuwa hakuna ulazima kwa Msanii kufanya kazi na Wasanii wakubwa ili kufanya vizuri au kutoka kwani kuna wasaniii wengine Wadogo na hawatambuliki lakini wanauwezo mzuri.

Siku ya tarehe 8 September 2013 Ben paul alifanya vitu vitatu ambavyo viulitengeneza Historia kwanza alikuwa akisharehekea siku yake ya kuzaliwa,pili alikuwa akitambulisha wimbo wake mpya ambao unakwenda kwa jina la #WAUBANI na Tatu ilikuwa ni kumtambulisha Msanii ambae alikuwa hajasikika katika Masikio ya watu wengi ALICE.

Alice ni msanii ambaye ameitendea haki kazi ya WAUBANI na kufanya vizuri kutokana na uwezo wake wa Sauti na namna ambavyo ameweza kuflow katika Uimbaji akishirikiana na Nyota wa RNB TZ.

Kupitia "Wa Ubani" utakubali kwamba Si lazima kufanya wimbo na Mastaa Tu, unaweza pia ukaimba na msanii mpya Aka-Fit vizuri #Beautiful'ALICE

0 comments:

Post a Comment