Raia
mmoja wa Canada amekamatwa nchini Colombia baada ya kujaribu kupanda
ndege kurejea Canada akiwa na tumbo bandia ya ujauzito alimokuwa
ameficha dawa ya kulevya aina ya Cocaine.
Mwanamke
huyo aliyekuwa anajifanya kuwa mtalii akirejea Toronto, alihojiwa na
polisi katika uwanjwa wa ndege wa Bogota aliyemshuku na kumuuliza
alikuwa amesalia na miezi mingapi kujifungua.
Alijibu
kwa ukali mno , hali iliyomfanya afisaa huyo kumshuku sana na hivyo
kumfanyia ukaguzi zaidi.
Afisaa
huyo aligusa tumbo lake na kuhisi ilikuwa baridi mno na ngumu sana
ndiposa wakaamua kumkagua zaidi.
walimpata
na dawa za kulevya zilizokuwa zimefungwa ndani ya tumbo bandia ya
mimba ambayo mwanamke huyo alikuwa ameivaa kwa kufunga tumboni.
Inasemekana
kuwa alisema ana miezi saba ya ujauzito lakini baada ya polisi
kumkagua walimpata na Cocaine kilo mbili iliyokuwa ndani ya vipochi
viwili
Mwanamke
huyo atashtakiwa kwa kosa la ulanguzi wa madawa ya kulevya na huenda
akafungwa jela kwa miaka mitano au nane.
Mwaka
huu pekee karibu watu 150 wamekamatwa na madawa ya kulevya katika
uwanja wa ndege wa Bogota.
Karibu
thuluthi moja ya waliokamatwa walikuwa raia wa kigeni, kwa mujibu wa
maafisa wakuu nchini Colombia.
source:BBC Kiswahili







0 comments:
Post a Comment