Thursday, September 12, 2013

DIAMOND AKANUSHA KUHUSIKA NA MADAWA YA KULEVYA,KUZAA NA MWANAFUNZI NA KUIBA WIMBO.

Msanii anaetamba na kufanya vizuri kwa ngoma ya My NumberOne ambayo imetengenezwa na produza Sheddy Clever amefunguka na kusema kuwa amesikitishwa sana na mambo ambayo amekuwa akizushiwa SIKU ZA KARIBUNI IKIWA NA PAMOJA NA KUANDIKwa kuwa anajihusisha na madawa ya kulevya,Kuiba nyimbo na issue ya Kuzaa na Mwanafunzi wa Kidato cha Nne.

 siku za karibunbi kumekuwepo na taarifa mbali mbali juu ya Mwanamuziki Diamond Platnum kuwa anajihusha na Biashara ya kuuza na kusafirisha Dawa za kulevya ambazo zinamfanya asafiri mara kwa mara Nchi mbalimbali.

Juu ya sakata hili Diamond Platnum amekanusha Tarrifa hizo na kusema kuwa yeye ajihusishi na Biashara hizo kabsaa wala hafahamu chochote juu ya Biashara hiyo bali amekuwa akipakaziwa tu pia amesema kuwa kipato akipatacho kinatokana na kazi yake ya Usanii na si kitu kingine.

Pili kulikuwa na Taarifa za yeye kuiba Wimbo wa Msanii Dyana Baba Levo ambao walikuwa wakilaumu kuwa Mwanamuziki huyo amewaibiwa Wimbo.

Platnum amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa kulikuwa na makubaliano mazuri kati ya Dyana na Produza Sheddy Clever ambae awali alimpa biti hiyo Dyana zaidi ya mwaka moja uliopita lakini ilionekana alishindwa kuifanyia kazi ndipo Produza huyo alipoamua kumpa biti hiyo Diamond Platnum na yeye kufanya unyama wake katika Ngoma hiyo.

MAHUSIANO YAKE NA PENNY alipohojiwa juu ya mahusiano yake na Mwanadada Penny amefunguka na kusema kuwa Ule ndio moyo wake hivyo ataendelea kumjali na kumtunza .


0 comments:

Post a Comment