Thursday, September 12, 2013

HAWA NDIO MAFISADI POLISI WANAOGOPA KUWAKAMATA.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, ameiambia  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa polisi hawajafanikiwa kuwakamata na kuwa tia mbaroni Mkuu wa..!
Kitengo cha Habari, Wizara ya Fedha,  Ingiahedi Mduma na Mkurugenzi wa Kampuni ya And- Line (2000) International, Daniel Ukwaya,  ambao wanakabiliwa na kesi ya  za ufisadi.

Wakili huyo alidai kuwa  upelelezi umeshakamilika na  kwamba itaendelea kutajwa kwa ajili ya kusubiri washtakiwa hao kukamatwa ili waunganishwe na wenzao na kusomewa maelezo ya awali kwa pamoja.


Kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi  na ufujaji wa fedha za utoaji wa matangazo na habari kwa vyombo mbalimbali vya habari.

Wanashtakiwa pia  kwa matumizi mabaya ya madaraka, mashtaka manane ya kughushi, shtaka moja la ubadhirifu na shtaka moja la kusababisha hasara ya Sh. Milioni 19.8.

0 comments:

Post a Comment