Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani humu, Lissu alisema maofisa wa
polisi wamesema bado wanaendelea na upelelezi na watawajulisha
watakapokuwa tayari.
Lissu
alisema baada ya kufika polisi na Sugu, maofisa polisi waliwaambia
kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Kwa
upande wake, Sugu alisema tukio hilo halitamrudisha nyuma bali
ataendelea kupigania haki za wananchi wake.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Sugu kudaiwa kumjeruhi askari wa Bunge katika
vurugu zilizotokea bungeni mwishoni mwa wiki iliyopita.







0 comments:
Post a Comment