Zikiwa
zimepita Siku kadhaa toka kutangaza kustaafu kufanya kazi ya Muziki
kwa Mzee Muhidini Gurumo na kuzawadiwa Gari na msanii wa BongoFleva
Diamond
Platnum Serikali nayo imekumbuka Mchango wa Mzee Gurumo
katika tasnia ya muziki kwa kumkabidhi Mzee huyo Barua kama kutambua
kazi aliyoifanya toka akiwa kijana.
Tukio
hilo lilifanyika Nyumbani kwake hivi karibuni nyumbani kwake
Makuburi, Jijini Dar es Salaam.
Katika
Picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi. Lilly
Beleko kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
akimkabidhi Mzee Muhidini Gurumo barua kama ishara ya Serikali
kutambua mchango wake uliotukuka katika tasnia ya Muziki nchini
pamoja na kumpongeza kwa kustaafu kazi kazi hiyo.
Wanaoshuhudia
nyuma ya Mkurugenzi ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Bw.
Addo Mwasongwe na kulia pembeni ya Mzee Gurumo ni Mkewe, Bibi. Pili
Said Kitwana.







0 comments:
Post a Comment