Chama cha Majaji
Wanawake kimesema kuwa katika Tanzania Rushwa ya Ngono inawaathiri sana Wanawake Maofisini kwani baadhi ya Waajiri
wamekuwa...!
wakitumia Madaraka yao vibaya kuomba Rushwa ya Ngono na
kuahidi kutoa ajira, kupandisha cheo, au kuongeza posho.
kimesema rushwa ya
ngono bado ni tatizo kubwa ambalo limeshamiri katika ofisi nyingi
hapa nchini.
Mwenyekiti wa chama
hicho, Angela Kileo alisema waathirika wakubwa wa tatizo hilo ni
wanawake maofisini, viwandani, mashuleni, vyuoni, majumbani na sehemu
nyingine za uzalishaji na utoaji huduma.
Licha ya vitendo hivyo
kushamiri kwa kasi kubwa Maofisi lakini kumekuwa na Usiri mkubwa
kwakuwa vitendo hivyo vinafanyika kwa usiri mkubwa mbali na
kutowatendea haki na kuwadhalilisha wanawake, lakini pia vinawaathiri
kimwili na kisaikolojia.
Kileo aliongeza kuwa,
licha ya athari zinazowapata kutokana na tatizo hilo, lakini wengi
wao huogopa kuripoti katika vyombo husika kwa kuhofia kupoteza ajira.







0 comments:
Post a Comment