Msanii mkali anaetamba
katika Tasnia ya BONGO Movie na Bongo Fleva Hemmedy PHD Ameweka wazi
kuwa kuanzia sasa hata vaa tena Hereni katika kazi zake za Muvi kwani
moja anaona amekuwa hivyo anahitaji kuonesha utofauti kati ya sasa na
zamani..!
Suala la kuvaa kwa
Hereni kwa Msanii Hemedy PHD lilionekana kuwakera Fans wake wengi
kwani hata Siku alipokuwa akichat Live Kupitia Ukurusa wa Facebook wa
#EATV Kupitia KIKAANGONI LIVE CHAT Mashabiki zake wengi walimuuliza
swali hilo la yeye kuvaa Hereni na kumshauri kuwa angeacha kwani muda
mwingine ilikuwa akipunguza Ufanisi wa Kazi yake ya Uigizaji katika
Baadhi ya SCENE.
Walimueleza kuwa
anaweza kuuvaa uhalisia lakini inapokuja suala la uvaaji wa hizo
Hereni inapunguza umakini kwa matazamaji kutokana na jinsi ambavyo
anakuwa amejiweka.lakini aliahidi kuwa atabadilikia siku moja na
kuaachana na Uvaaji wa Hereni hizo.
Kutokana na Kusikiliza
Mawazo ya Mashabiki zake Hatimaye Mwanamuziki huyo na Muigizaji
ametangaza Wazi kuwa hawezi kuvaa tena Hereni hizo katika Kazi zake.







0 comments:
Post a Comment