Baada ya baraza la
wazee wa Yanga kupinga maamuzi ya uongozi wa klabu yao kumuajiri raia
wa Kenya, Patrick Naggi, kuwa katibu mkuu mpya klabu hiyo wanachama
wengine wa Yanga wamefunguka na kusema...! kuwa Wazee wa Klabu wanataka
kuivuruga Timu na Uongozi kiujumla kwa sababu wao hawaoni kama kuna
tatizo kwa Raia huyo wa Kenya kuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga
kwani hata Kocha na baadhi ya wachezaji si Raia wa Tanzania lakini
kwa kuwa wanauwezo wa ziada ndio maana wakawepo hapo.
"Baadhi ya wazee
hawa wana kawaida ya kuibua baadhi ya mambo ili waitwe na uongozi
kisha wapozwe na chochote ili waache chochoko ambazo hazina msingi
klabuni kwa manufaa ya klabu," alifunguka mwanachama mmoja.
Katibu Mkuu wa Baraza
la Wazee wa Yanga, Yahaya Akilimali, alisema kuwa hawakubaliani na
uteuzi huo wa raia wa kigeni kushika nafasi hiyo wakati wapo
wazalendo wenye elimu na uwezo kwa kuiongoza Yanga na kuipa mafanikio
makubwa tu.
"Ni kama
wametudhalilisha, wapo vijana wetu wasomi na wenye uwezo kushika
nafasi hiyo, hatukubaliani na uteuzi huu, kwa nafasi hii nyeti
inahitaji mtu mwenye mapenzi na Yanga,"






0 comments:
Post a Comment