Wednesday, September 4, 2013

BABA LEVO AMEIBUKA NA KUSEMA DIAMOND PLATNUM KAMUIBIA KIITIKIO CHA WIMBO WAKE.

Msanii Baba Levo mzawa wa Kigoma na anaewakilisha kundi la Kigoma AllStars leo amefunguka na kusema kuwa Msanii Diamond Platnum ameiba Chorus ya Wimbo wake unaokwenda kwa Jina la SWEATY SWEATY.

Maelezo ya Baba Levo ni haya hapa

ZAMANI nilikuwa nikiskia mtu analalamika kaibiwa wimbo au kaibiwa njia. Nilikuwa naona ni kama maigizo na mtu kutafuta kick ya kupandia .

ila leo nasema wazi DAIMOND PLATNUM amechukua korasi ya wimbo wangu niliopanga kufanyanae unaitwa SWEATY SWEATY na kuiimba kwenye wimbo wake mpya NO 1 .. 
 
kanizungusha sana kumbe alikuwa na lengo lake...ila baridaa maisha yanasonga..”Mwisho wa Kunukuu .

kama kweli hili lipo hapa naweza kusema kweli Diamond kaiba wimbo maana ni ubunifu wa Msanii katika Chorus ila Beat Hapana si miliki ya Msaniii.



0 comments:

Post a Comment