Friday, September 6, 2013

KUKUTANA KWA KIKWETE NA KAGAME KUMEONDOA HOFU KUBWA ILIYOKUWEPO

Rais Jakaya Kikwete jana amekutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame katika mazungumzo yaliyobainishwa kuwa yalikwenda vizuri na kuisha vizuri...!
Kwa mujibu wa Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais iliyotolewa jana ilisema mazungumzo kati ya Viongozi hao Wakuu wa Rwanda na Tanzania yalidumu kwa zaidi ya saa moja yalikidhi haja na tija za pande zote mbili.

“Viongozi hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa Kampala, Uganda, “


Kwa mujibu wa Taarifa hiyo Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Hofu ya Vita imepungua kwa namna moja au Nyingine kutokana na Viongozi hao kutumia busara kutatua Tofauti zilizokuwa zikifanya Nchi hizi kuwa katika wakati mgumu wa mapito kwa kutofautiana Kidiplomasia na kutumiana maneno ya Vijembe ambayo yalikuwa yanatoa Ishara Mbaya kwa Wananchi wa Nchi zote kati ya Tanzania na Rwanda.

0 comments:

Post a Comment