Mtu mmoja aliyefahamika
kwa Jina la Alex Sumni Massawe (33), alikamatwa jana Majira ya Saa
tano za Asubuhi katika Hospital ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi akiwa
katika Maandalizi ya Kumfanyia Upasuaji Mgonjwa..!
ambae amefahamika kwa
Jina la Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa Ngozi.
Habari zinasema kuwa
kabla ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi wa kijana huyo, mkazi wa
Manispaa ya Moshi, Pamvelina Shirima, alikutana na mtuhumiwa huyo
katika baa moja maarufu mjini hapa iliyopo eneo la Dar Street na
kumtaka ampe kiasi cha Sh. 200,000. cha fedha kwa madai zitatumika
kuharakisha mwanaye wa kiume kufanyiwa vipimo vya upasuaji.
Ofisa Uhusiano wa
KCMC, Gabriel Chisseo, alisema kuwa daktari huyo aliwekewa mtego na
uongozi wa hospitali hiyobaada ya baadhi ya wagonjwa kuripoti
kutapeliwa na mtu ambaye amekuwa akijitangaza kwamba ni daktari wa
“Huyu Alex Massawe tulimkamata leo (jana) asubuhi akiwa
katika wodi ya upasuaji baada ya kupokea kiasi cha Shilingi 200,000
kutoka kwa Pamvelina Shirima ambaye alimleta mwanaye afanyiwe
upasuaji wa ngozi.
WITO WETU Tunawataka wagonjwa wote kufuata
taratibu ikiwamo kutokubali kurubuniwa na watu ambao hawajavaa sare
wala kuwa na vitambulisho rasmi vya hospitali,” alisema Chisseo.







0 comments:
Post a Comment