Lakini
Taifa Stars inakwenda Gambia ikiwa dhaifu kwa kuwakos wachezaji nyota
ya Timu hiyo zaidi ya Saba ambao huwa katika First Eleven ambao wengi
wao ni Majeruhi huku Nyota wengine hawajaweza kutokea katika Kambi ya
bila kuwapo kwa taarifa yoyote ile.
Kocha
Kim Poulsen wa Taifa Stars aliwataja wachezaji hao aliowahitaji sana
kwa mechi dhidi ya Gambia itakayochezwa Jumamosi lakini wakakosekana
kutokana na sababu mbalimbali kuwa ni Shomari Kapombe, Kelvin
Yondani, Aggrey Moris, Salum Aboubakar 'Sure Boy', Athumani Iddi
'Chuji', John Bocco na Mwinyi Kazimoto.
Pia
aliwataja nyota wengine kuwa ni wachezaji wa TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu; ambao hadi
jana mchana walikuwa hawajawasili nchini na hakukuwa na taarifa
zozote rasmi kueleza sababu zilizokwamisha ujio wao.
Mbali
na Hao Stars Imemkosa Mwinyi Kazimoto aliye temwa kwa utovu wa
nidhamu baada ya kutoroka kambini Kipindi wakijiandaa kucheza dhidi
ya Uganda .







0 comments:
Post a Comment