Habari
zilizopatikana kutoka Yanga zinaeleza kuwa Mkenya huyo amepewa
mkataba wa mwaka mmoja na ajira yake ilianza rasmi Septemba Mosi.
Kwa
upande wake Mwalusako alisema kwamba yeye anachofahamu ni kwamba
amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja aliopewa na hajapewa maelekezo
mengine na uongozi wa klabu hiyo pia aliongeza kwamba hana tatizo
lolote na viongozi wake na kwamba yuko tayari kupokea maamuzi yoyote
ambayo watayafanya dhidi yake.
Afisa
Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kwamba hafahamu chochote na
yeye bado anamtambua Mwalusako kuwa ndiye katibu mkuu wao.
Baaada ya sakata hilo wazee wa Yanga yamemkataa Patrick Nagi kuchukua nafasi ya Mwalusako kwa kigezo kuwa hapa Tanzania kuna watu wengi wenye uwezo wa juu wa kufanya kazi hiyo na sii huyo Patrick ambaye ni raia wa Kenya.







0 comments:
Post a Comment