Wednesday, September 4, 2013

HALI YA UTAYARI KIJESHI IMEPANDA TANZANIA LOLOTE LAWEZA TOKEA.

Kwa mujibu wa Jeshi la Wananchi Tz kupitia Account yake ya Twitter limetangaza hali ya utayari kijeshi katika Jeshi la Kulinda Amani Tanzania JWTZ na kusema kuwa hali hiyo imepanda kutoka Asili 25% ambayo huwepo Nchi iwapo katika Amani na Utulivu.

 Kwa mujibu wa Mtandao wa Kijamii wa Twiteer ambao ni Jeshi la Wananchi Tz@JW_TZ umetoa taarifa kuwa kwa sasa Nchi ipo katika Utayari wa Kijeshi kwani wameahirisha likizo zote za wanajeshi wa Tanzania na wale waliopo likizo wameamriwa kurejea Makambini kwao kuwa tayari kwa lolote.

Tumeahirisha likizo zote za wanajeshi wetu, na waliokuwa likizo wameamriwa kurejea, tumepandisha hali ya Utayari wa Kijeshi kutoka 25-50”

Kutokana na Mazingira yaliyopo Asilimia za Utayari zimepanda tena kutoka ile 50 iliyotangazwa awali
Katika hali ya amani na utulivu katika nchi, hali ya Utayari Kijeshi huwa kwenye 25%. Na katika hali ya vita kamili huwa ni 100%”

Jeshi hilo limetoa kauli kuwa baadhi ya Brigedia zilizopo Tabora zimeshapewa agizo kuwa katika hali ya Utayari kwa jambo lolote lile.
Brigedia za Tembo na Kifaru (Tabora) tayari zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari wakihitahitajika kufanya jambo lolote la kijeshi “


0 comments:

Post a Comment