Kutokana
na kukua kwa Jiji la Dar es Salaam, na katika hali ya kutaka klabu
iwe na vitega uchumi klabu imeonelea ni vyema kama ingekuwa na uwanja
wa mpira
wa karne ya sasa na baadaye ambao pamoja na mambo mengine
utakuwa na mioundombinu ifuatayo:-
1. Uwanja
wa mpira wenye viti 40,000
2. Hostel
ya wachezaji na football academy ya vijana
3. Viwanja
vya mazoezi
4. Uwanja
wa kutosha kuegesha magari
5. Hoteli
na sehemu ya makazi
6. Ukumbi
wa mikutano
7. Sehemu
ya maofisi, benki, zahanati (sports clinic)
8. Maduka,
supermarket na sinema
9. Sehemu
za kubarizi, kupumzikia (Recretional and Open spaces)
Mara
baada ya azma yetu kukamilika eneo hili litaitwa “Jangwani City”
na kufanya wakazi wa maeneo ya Jangwani na sehemu za jirani wasiende
maeneo ya mbali kutafuta huduma muhimu za kijamii. Eneo hili
litaboresha mandhari nzima ya Jangwani kwa kukuza mazingira na
miundombinu. Hii itahusu pamoja na mambo mengine ujazaji udongo (tuta
kubwa), upandaji miti, bustani za kubarizi, kuboresha mifereji ya
majitaka na kudhibiti mafuriko ya eneo la Jangwani na hivyo kulipatia
sura ya kibiashara na kitalii.
Ili
kukamilisha azma ya kuwa na Jangwani City itakayo kuwa na miundombinu
yote hiyo, Uongozi ulipeleka maombi ya eneo la nyongeza Manispaa ya
Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa barua
zenye kumbukumbu namba YASC/ARDHI/MWK/YM/46/2012 na
YASC/ARDHI/MWK/YM/47/2012 za 12 Desemba 2012, na mpaka sasa bado
maombi yetu hayajajibiwa.
Mwezi
wa saba, Wadhamini/Uongozi wa YANGA walimwandikia Mheshimiwa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam kuomba msaada wake kufanikisha maombi ya
nyongeza ya kiwanja yaliyowasilishwa Manispaa ya Ilala na Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Klabu
ya Yanga ina kiwanja chenye ukubwa wa hekta 3.59 eneo la Jangwani.
Kiwanja hiki kina hati miliki kwa miaka 99 toka mwaka 1972 na katika
eneo hilo, klabu ilifanikiwa kujenga uwanja wa mpira wa Kaunda na
Jengo la klabu la ghorofa tatu. Jengo hili lilijengwa kwa ufadhili
mkubwa sana wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani
Karume (Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi) na michango ya
wanachama na wapenzi wa klabu ambao kila siku wamekuwa wakiamini kuwa
haba na haba hujaza kibaba.







0 comments:
Post a Comment