Wednesday, September 18, 2013

PRISONS YAPANIA KUINYOA YANGA LEO

Wakati Kocha wa Yanga, Ernest Brandts akitegemea kumuanzisha kiungo wake nyota Haruna Niyonzima 'Fabregas' kwenye mechi ya leo ya Ligi Kuu ya Bara..!
dhidi ya Prisons, kocha wa Prisons Jumanne Chale amepania kuwanyoa Mabingwa hao na kuondoka na pointi tatu kwenye mechi hiyo ya kwanza kwenye uwanja wa nyumbani.

Brandts amekili kuwa kukosekana kwa nyota ambae ni raia wa Rwanda Niyozima kulichangia kutoka sare na Mbeya City lakini kwa kuwa amerejea naamini mambo yatakwenda sawa.

“Kikubwa kwangu ni kurejea uwanjani kwa Haruna. Hakuwapo kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Mbeya City.. lakini leo atakuwapo. Lengo letu ni kushinda ili tuondoke na pointi nne huku japo najua kuna ugumu wake kwa sababu Prisons wamejiandaa vizuri,” Brandts.

0 comments:

Post a Comment