1:24 AM

SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG
23)
Hivi karibuni kuna mtu unaetaka kukutana nae lazima mtakutana
lakini itakubidi umfuate,na uzungumze naye, kwani hakuna la maana
utakalolipata usipomfuata. Mipango itatimia tu baada ya kukutana nae.
MASHUKE – VIRGO(AUG 24- SEPT 23)
Kuna Mtu atakuja leo
kukusaidia, akija mwinukie, atakuwa anatoka upande wa Magharibi au
Kusini na atakuja muda wa jioni, Jihadhari kuna mikakati mibaya
inaundwa juu yako, unashauriwa kuhama mji au kubadili kazi yako ya
sasa
MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Mchana huu kuna
mtu utakutana nae, mtu huyo anaweza kuwa mpenzi, anaweza kuwa mpenzi
au mtu mtakaesikilizana sana. Mpokee na kuwa nae utafanikiwa na
atakuinua sana kimaisha. Kuna habari za sherehe utapokea katika
kipindi cha siku mbili.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Kama
leo mchana kama unamipango na mtu yoyote usione shaka kumkabili,
mwelezee na mambo yako yatafunguka japokuwa yatakuwa na hasara kubwa
na faida kidogo usikate tamaa huo ni mwanzo tu, baadaye mambo yako
yatakuwa mazuri sana.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Leo kuna dalili ya kutokea matokeo ya kutatanisha au kupotelewa
na vitu vyako kiajabuajabu. Utapata habari ya kifo na Unaweza
uchanganyikiwe. Unashauriwa kuwa mvumilivu kwani kifo hiki ndio
ufunguo wa bahati yako.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo usione tatizo kumtolea mtu wako wa karibu shida zako utapata
haja yako mara moja kama si leo, itakuwa Jumatatu ijayo au Mwezi wa
Septemba lakini itatimia.
Elewa kuwa mfanyakazi wako wa ndani au
msaidizi wako katika kazi au biashara amegundua siri zako na ana
mpango wa kuzitangaza. Muwahi kabla hujadhurika.
NDOO
–AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Kuna wasiwasi kuwa utapata
maradhi ya kifua ambayo yatakusumbua sana lakini mwishowe utapona kwa
msaada wa rafiki yako.Jaribu kuwa nyumbani nyakati za jioni jiepushe
na safari za usiku kuepukana na upepo mbaya utakaokuingia
kifuani.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Pana mtu
anaitwa Yusufu au Joseph au jina lake linaanza na mojawapo ya herufi
zilizo katika majina hayo atakusaidia na lazima ushirikiane
nae.mtafute na utapata faida kubwa.
PUNDA- ARIES (MACH 21-
APR 20)
Leo kama kuna mtu unayetaka kushirikiana nae jina lake
linaanza na moja ya herufi hizi ‘ ‘S’, ‘F’, ‘P’, ni
vizuri zaidi.Mtu huyo atakusaidia kugundua njama unazofanyiwa na
jamaa zako wa karibu, unashauriwa kujifanya kama hujazijua njama zao
ili kuzipata za ndani zaidi.
NG’OMBE – TAURUS (APR21 –
MAY 20)
Mchana huu Pendelea sana kumsifu kila utakae kutana nae
utaona ajabu. kwamba mambo yako yatanyooka na kufanikiwa kwa hali ya
juu sana, unashauriwa kuwa mtu wa ibada na kutoa sadaka.
MAPACHA
- GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Mchana huu una mawazo sana kuhusu Ndoa
au Mwanamke au Mwanamme. Mambvo hayo yatafunguka baada ya siku saba .
Unatahadharishwa usijishughulishe na ugomvi wowote utakatokea hapa
mtaani kwako hata kama ni mtoto wa jirani yako, kwani kujiingiza
kwenye ugomvi huo ni kujitakia balaa kubwa.
KAA – CANCER
(JUN 22 – JUL 23)
Leo Karibisha wageni, fanya vitendo vizuri
saidia sana haja za watu
na itakufanya ufanikiwe katika mipango
yako au matibabu yako au ya jamaa yako aliyeugua kwa muda mrefu..
Mgonjwa akipona toa sadaka.
0 comments:
Post a Comment