SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Jumanne
ya leo jitihada zako ndizo zitakazokufanya wewe kufanikiwa kirahisi,
jaribu kuwa karibu na watu wa dini ili kubrilikiwa mambo yako.Kazi
nyingi nzito na ahadi kibao zisizitekelezeka zinaweza kuwa
kikwazo.
MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Leo hii ni
siku muhimu sana kwako kuwa muangalifu, faida utakayopata katika
mambo yako isikufanye ukabweteka na kufanya dharau kwa watu
wengine,ikitokea siku ya leo ukikutana na mtu ambaye hana miguu
kabisa, hiyo ni dalili kuibiwa mali yako au kupoteza vitu vya thamani
kubwa,
MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Leo fanya
uchunguzi wa mambo unayoyatilia mashaka, jaribu kuwa karibu na wale
ambao unahisi wanaweza kukupa msaada jihadhari na vikundi visivyofaa
hasa nyakati za jioni. Jaribu kuwasiliana na wataalamu ili
wakusaidie.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo
utafanikiwa baada ya kusumbuka kwa muda mrefu tumia utakachopta
kutumia na wengine usiwe mbahil, lakini elewakwamba mambo yako yamo
hatarini kuharibiwa na watu, unatakiwa kuwa mpole kwa muda huu ili
kupisha dhahama hiyo.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 23)
Siku ya leo usipokuwa makini kipato chako kitapotea bila kujua na
wiki hii unashauriwa kutosafiri ili kujikinga na mabalaa katika
safari hizo. Jaribu kuwa muangalifu na yoyote utakayeshirikiana naye
ili kuokoa kile ambacho kitasalia
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 –
JAN 20
Leo hii tafuta njia zaidi za kukusaidia, marafiki na
majirani wa karibu wanaweza kutoa mchango mzuri , kuna dalili ya
kufanikiwa katika mambo yako, unashauriwa kuutumia muda huu
kukamilisha mambo yako uliyokuwa umeyapanga kuyafanya.
NDOO
–AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 39)
Leo ni siku mbaya kwako
inaonekana shughuli zako zinaweza zikakumbwa na dosari kuna uwezekano
wa kupata mkosi kazini kwako au utaletewa biashara ambayo itakuletea
balaa kimaisha. Jaribu kuwa muangalifu mipango yako yote uliyoipanga
hasa leo achana nayo.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo
hii katika biashara zako utapata faida ambayo hukuitegemea na yule
rafiki yako uliyemkosea utakusamehe madhambi uliyomfanyia. Jitahidi
kukutana na wakubwa zako wakusaidie kupata ushauri.
PUNDA-
ARIES (MACH 23- APR 20)
Pamoja na kwamba leo inaweza kuwa siku
njema kwako utapatwa na mambo ya ajabu ajabu, mambo hayo
yatakushangaza usijaribu kujibishana na watu usiowajua kunaweza
kutokea ugomvi mkubwa.tegemea kupata safari ya itakayokupeleka sehemu
ambayo hujawahi kufika.
NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY
20)
Usiendekeze mambo makubwa kwani unaweza kujikuta ukiingia
kwenye matatizo na kupata hasara, upo uwezekano wa kukutwa na balaa
huko uendako.kuna uwezekano wa kutokea matatizo kazini kwako au kwa
mtu anayekuhusu,
MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Vikwazo
havitakosa kukuandama siku ya leo unaweza kujikuta hata wale
uliowategemea sana katika utekelezaji wa mambo yako nao wakakuweka
kwenye wakati mgumu
KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
yoendelea kukupotezea
Jumanne ya leo usisumbuke na mambo madogo
madogo ambayo yanayoendelea kukupotezea mudaa ni wakati wa kuangalia
mbele, uhusiano wako na mtu uliyempata hivi karibuni awe ni mpenzi au
rafiki utavurugika, Unashauriwa kuwa makini na hao marafiki wapya
watakaokujia siku za karibuni.
Mtabiri Maalim Hassan
YahyaHussein anapatikana Dar-es-salaam kila siku Ofisini kwake
Magomeni Mwembe Chai, karibu na Kituo cha Mafuta cha SOPCO (Zamani
BP). Simu 0754 672464
0 comments:
Post a Comment