Tuesday, August 6, 2013

BAADHI YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAKILI KUFANYA BIASHARA YA KUUZA MIILI YAO USIKU.

Baadhi ya Madada poa wanaofanya kazi ya kuuza miili yao katika kumbi mbalimbali za starehe wanajitambulisha kuwa ni wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kama vile Chuo cha.....!
Ustawi wa Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo ca Biashara (CBE), ingawa ni ngumu kuthibitisha ukweli wa kile wanachosema, lakini inaaminika lengo ni  kuongeza thamani.

Huduma ya wahudumu hao wengine huwaita ‘changudoa’ au ‘dada poa’ inatofautiana kwa gharama. Inapanda na kushuka. Ni kama biashara ya wamachinga kutumia neno na wewe, ‘unazungumza’ wanapokuwa katika majadiliano na mteja.

“Showtime ni 20 tu; na kama ni hadi asubuhi 50.” Hii ni bei inayotolewa na Amina kwa upande wake anapokutana na mteja.

Dar es Salaam, tabia hiyo inafanyika katika maeneo mengi kuanzia saa 4 usiku hadi kunakucha.

Baadhi ya watu walioishi miaka mingi,  wanakumbuka kwamba tabia ya wanawake kuishi Dar es Salaam kwa kuuza miili iliibuka mapema miaka ya 1970.

“Wakati huo biashara ilikuwa inafanyika  vibandani kwenye mitaa mbali mbali ya mafichoni,” anasema mmoja wa kazi wa Temeke huku akiomba kuhifadhiwa jina lake.

Lakini sasa, Mzee huyo anasema mbali na kumbi za starehe kutumika kama mtego wa kunasa wateja, biashara ya kuuza miili Dar es Salaam inaanza muda mfupi mara tu baada ya jua kuchwa.

“Kasi ya biashara hiyo ni kubwa, changudoa wanajipanga mitaani kunasa wateja kwenye magari yanayopita barabarani, tofauti na zamani walipokuwa wanafuatwa vibandani,” anasema.

Mbali na Klabu Ambiance, iliyopo Barabara ya Shekillango wilayani Kinondoni, biashara hiyo imeshika kasi kubwa pia katika maeneo mengi ya wilaya za Temeke na Ilala.

Kwa wilaya ya Kinondoni maeneo hayo ni pamoja na Sea Cliff, Oysterbay, St. Peter’s, Super Market huko Msasani na Makaburini karibu na soko liitwalo la kimataifa - Kinondoni.

Kwa upande  wa Temeke ni maeneo ya karibu na mtaa wa Wailes wakati huko Ilala, mitaa inayotajwa kuwa maarufu kwa biashara hiyo ni pamoja na Ohio huku mingine mingi ikiwa sehemu za Buguruni.

Wanapokuwa wamejipanga kandokando ya barabara wakiwa nusu utupu, wasichana hupunga mikono kama anavyofanya mtu anayesubiri usafiri, lakini magari yanaposimama wanayavamia huku wakitangaza bei ya huduma yao.

Huduma yenye bei ya chini kuliko zote ni ngono kupitia sehemu ya kawaida ya siri ya mwanamke, inayofuatiwa na ya kupita ‘mlango wa nyuma’ na yenye gharama kubwa zaidi ni ile ambayo inatolewa kwa njia ya midomo.

Ingawa wanaofanya biashara hiyo wanaonekana ‘kujali’ kwa kuwasisitizia wateja wao kuvaa mpira wakati wa tendo la ngono ya kawaida, baadhi ya wateja wao wanasema makahaba wengine hawafanyi hivyo wanapotoa huduma kwa njia ya mdomo na ya mlango wao wa nyuma, kwani wanachojali ni dau kubwa tu.

0 comments:

Post a Comment