Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amefunguka na kusema kuwa
amechoswa na Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA)
kutokana na kushindwa kufanya kazi yao ipasavyo na kushindwa kuwalipa
wafanyakazi wa Shirika Hilo.
“Nimechoshwa
na menejimenti ya Tazara, wanashindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi
halafu wanaendelea kuwapo, mna mabilioni ya fedha mnawadai watu
halafu mnashindwa kukusanya,” alisema Dk. Mwakyembe.
Waziri
huyo wa Uchukuzi ameipa miezi mitatu menejimenti ya Shirika la Reli
la Tanzania na Zambia (Tazara), kuwalipa wafanyakazi malimbikizo ya
mishahara zaidi ya Sh. milioni 624.4 kwa wakati na wakishindwa waache
kazi.
0 comments:
Post a Comment