Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema Tendwa alipaswa kuwa
ameondoka kwenye Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa tangu mwaka 2008
alipofikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Chadema ilisema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotumwa na Ofisa Mwandamizi wa Habari wa chama hicho.
Alidai kuwa Tendwa aliendelea kufanya kazi zake hata baada ya muda wa mkataba wake alioongezewa kuwa umefikia mwisho. “Hivyo, alikuwa anakalia ofisi hiyo ya umma kinyume cha sheria,”
mbali na hilo, Tendwa alitumia muda wa miezi kadhaa aliokuwa anakalia ofisi ya umma kinyume cha sheria, kuropoka, kuharibu demokrasia, kwa manufaa ya serikali na CCM.
Kwa mujibu wa Makene, kutokana na mwenendo wake mbovu, Chadema ilitangaza kutokumpa ushirikiano wowote, yeye kama Tendwa, ikiwa ni pamoja na kumtangaza kuwa adui wa demokrasia nchini. Hata hivyo, alisema kwa muda wote huo, Chadema ilikuwa ikitoa ushirikiano kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Alisema badala ya kuifuta Chadema na kufanikisha dhamira ovu ya kuharibu amani ya nchi, ameondoka yeye.
0 comments:
Post a Comment