Mbunge
wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji ameachiwa huru dhidi ya kesi ya
Uchochezi iliyokuwa ikimkabili,ambayo ilifunguliwa na Serikali...!
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara jana ilitupilia mbali shitaka la kesi
hiyo ya uchochezi wa vurugu za kupinga kujengwa bomba la kusafirisha
gesi asilia .
Sababu
za Hakimu kufuta mashtaka yaliyokuwa yakimkabili Mbunge huyo ni
pamoja hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani hapo kuwa na
upungufu mkubwa wa kisheria.
Wakili
Peter Kibatala,ambae ndie alikuwa akimtetea mbunge wa Mtwara
Mjini,alidai miongoni mwa upungufu uliokuwamo kwenye hati hiyo, ni
pamoja na kutokuwa na maelezo yanayoonyesha waziwazi kosa alilokuwa
akishtakiwa mteja wake.
0 comments:
Post a Comment