Friday, August 2, 2013

KITANZI CHA YANGA DHIDI YA AZAM MEDIA CHAANZA KULEGEA.


Siku moja baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kutoa tamko kuwa kama Yanga itaendelea na msimamo wa kupinga au kukataa udhamini kampuni ya Azam Media ambayo imepewa dhamana ya kuonesha mechi zote za Ligi Kuu Bara katika Luninga klabu hiyo haitalamba.....!
mgawo wowote ule wa pesa.

Baada ya kauli hiyo Uongozi wa Yanga umesema kuwa tatizo la kwawo wao si pesa bali wao wanachokitaka ni kuwa na uhakika kama Klabu yao haitahujumiwa au kutotendewa ndivyo sivyo na wadhamini hao katika Ligi ambao nao pia ni wamiliki wa Timu ya Azam inayoshiriki ligi kuu Bara.

Mbali na hilo Kiongozi huyo aliendelea kufafanua kuwa wangependa kuona kuwa mdhamini wao kampuni ya bia Tanzania (TBL) itatendewa haki kama walivyokubaliana wakati mabingwa hao waliposaini mkataba.

"Tatizo letu si pesa, tunataka kuhakikishiwa kwamba hatutachakachuliwa na kumuweka TBL katika matangazo kabla na baada ya kumaliza mechi zetu," alisema kiongozi huyo.

0 comments:

Post a Comment