Ufisadi
wa Shilingi bilioni saba umebainika katika Chama Kikuu cha Wakulima
wa Tumbaku Kanda ya Magharibi...!
Imegundulika
kuwa, wakulima wamekuwa ‘wakiibiwa’ kwa mfumo wa kupelekewa
pembejeo ‘hewa.’ Madai hayo yamebainisha kwamba wanaonufaika na
wizi huo kwa wakulima ni vigogo wa Wetcu wakishirikiana na mawakala
wanaosafirisha pembejeo hizo.
Mwenyekiti
wa muda wa bodi ya Wetcu, Hassan Wakasuvi, alipoulizwa kuhusiana na
ufisadi huo alikiri kwamba kuna vyama vya msingi vinadai kwa kuwa
vililipa fedha, lakini havikupelekewa pembejeo huku vingine vikikatwa
misimu miwili bila kupelekewa pembejeo. “Vingine vilikatwa pesa
hata mbolea haikuwafikia, vingine vinadai pembejeo lala yaani
walilipa lakini hadi msimu wa kilimo unaisha hawajapata pembejeo.”
Kwa
upande wake, Kaimu Meneja Mkuu wa Wetcu, John Kusanja, alisema bodi
inahakiki deni hilo ili wawalipe wakulima. Alisema “kuna vyama
ambavyo vimelipa zaidi na vingine vililipa pungufu kwa hiyo
anayedaiwa atalipa na anayedai atalipwa.”
Waziri
wa Kilimo Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, alipoulizwa
kuhusiana na ufisadi huo alisema yuko kwenye mapumziko na kwamba
asingeweza kuzungumza lolote wakati huo.
0 comments:
Post a Comment