Monday, July 8, 2013

WAKAZI KAMUONESHA TID KILICHO MPELEKA BBA

Baada ya taarifa kuvuma kuwa Rapper kutoka Tanzania Wakazi ndie angekuwa mshiriki atakaefanya Show ya BBA katika Wkeend iliyopita ,Suala ya wakazi kuchaguliwa kwenda South Africa kama Rapper kutoka Tanzania liliibua maswali mengi kwa Watanzania walio wengi ambao walidai kutomfahamu wala kumsikia mwanamuziki huyo katika muziki wa Bongo.Lakini........


Msanii anaewakilisha Wanyama Alimaarufu kama Top in Dar (T.I.D) hakuwa nyuma katika kupigwa na bumbuwazi juu ya Msanii wakazi kwenda kupiga show kama Rapper wa Tanzania mpaka mtu mzima TID alihoji Wakazi ataimba wimbo gani, au anaenda kuonyesha kofia zake za marekani?

Wakazi nae alijipanga kuwaonesha watanzania na Dunia kiujumla kuwa yeye ni Rapper na kuwa alikuwa akistaili kufanya Performance hiyo katika jumba la Big Brother Africa,hivyo alifanya Show kali iliyoeleweka na kupokewa vizuri na Washiriki wa Jumba la Big Brother.

0 comments:

Post a Comment