Wewe
ni shahidi kuwa wengi wetu tunaingia kwenye mahusiano baada ya
mahusiano ya awali kuvunjika. Jambo hili sio baya na wala sio la
kushangaza kwasababu kila mtu anauhitaji wa kuitimiza kiu ya kupenda
na kupendwa ambayo ni hitaji la kimsingi kabisa la kila mwanadamu lakini........
kwawale
walio soma “Maslow’s hirachy of needs” watanielewa zaidi hapa.
Tatizo linakuja kwenye “tunaanzaje mahusiano haya mapya?” na “je
tumemalizanaje na yale ya awali?” Usiwe mwepesi kusema ndiyo
kumkubali mpenzi mpya au kufungua mlango kwa penzi jingine wakati
lile la mwanzo haujaufunga mlango ukafungika. Wengi wamejikuta wana
penzi pande mbili baada ya kuanza mahusiano na mtu mwingine wakidhani
walishamalizana nayule wakwanza,
tena
hawakuwa wazi hata kwa huyu mpenzi mpya kumtaarifu kwamba
ninakukubali ila kuna mtu bado hatujang’oa mizizi ili nayeye
ajiandae kwa chochote kitakachotokea kesho. Baadae unajikuta kwenye
njia panda inayoumiza sana moyo na kuleta msongo wa mawazo “stress”
tena kwa kujitakia tu.
Una
haraka ya kwenda wapi? Usitumie kuharakisha kuingia kwenye penzi
jipya kama maji baridi yakupooza maumivu yako ya penzi la awali.
Hakikisha umepona kwanza majeraha yako ya kwanza kisha ufanye maamuzi
halisi na thabiti ya kuanza tena mahusiano mapya. Kamwe usihusiane
kwa nia ya kupooza vidonda vya ndani maana vikisha poa utakuja
kugundua halikuwa penzi bali ilikuwa ni huduma ya kwanza tu.
Ingia
kwenye penzi ukiwa na uhakika na fanya maamuzi thabiti ili uwe tayari
kwa kila yanayotokea ndani ya penzi hilo. Kumbuka “We love in order
to stay, we don’t love in order to leave” - Mwandishi Chris
Mauki.
0 comments:
Post a Comment