1:10 AM

Mfanyabiashara
Heaven Kassia (44), mkazi wa Bahari Beach jijini Dar es Salaam,
anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kwa kosa la kuwagonga
kwa gari makusudi watu sita kutokana na kile kinachodaiwa kuwa wivu
wa kimapenzi.
Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova,
aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea Juni
30, mwaka huu, katika baa iitwayo Kilongawima Resort wakati mtuhumiwa
akiwa na rafiki yake wa kike aitwaye, Jovita Njunwa ambaye pia ni
mfanyabiashara.
Kova alithibitisha kuwa mfanyabiashara huyo
akiwa katika baa hiyo na rafiki yake huyo wa kike, meza ya pembeni
walikuwepo watu sita, ambapo baadaye Njunwa alihama kutoka katika
meza yake na kwenda kukaa nao.
Kwa mujibu wa Kova, baada ya
Njunwa kuhamia meza hiyo ilizuka tafrani kubwa kati ya Kassia na watu
hao sita, kiasi cha kuanza kurushiana maneno makali yenye ishara ya
kumgombea mwanamke huyo.
Alisema kuwa wakati huo Kassia
alikuwa akidai kuwa rafiki yake amekwisha mgharamia Njunwa fedha
nyingi, hivyo kuwataka wanaume hao wamwache bila maelewano.
Kova
alisema kitendo hicho kilisababisha Kassia kuwasha gari lake lenye
namba za usajili T 546 BXX aina ya Toyota Hilux na kuondoka kwa
mwendo wa kasi kuelekea katika ile meza ya wanaume hao na kuwagonga
kwa nguvu kiasi cha kuwasababishia majela sehemu mbalimbali za miili
yao.
Aliongeza kuwa watu hao walivunjika miguu, mbavu na
kuumia vichwani, hivyo kukimbizwa katika Kitengo cha Mifupa cha
Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako wamelazwa wakiwa mahututi.
Kova
aliwataja majeruhi hao kuwa ni Solomon Kirato, Peter Marwa, Yahaya
Albert, Noah na wengine ambao majina yao hayakufahamika.
Kwa
mujibu wa Kova, mtuhumiwa amekamatwa na uchunguzi unaendelea kuhusu
kosa hilo la kutaka kuua kwa makusudi pamoja na kosa la kujaribu
kujiua baada ya tukio hilo.
Alisema kuwa mtuhumiwa anatarajiwa
kufikishwa mahakamani baada ya jalada kupelekwa kwa Mwanasheria Mkuu
wa Serikal
0 comments:
Post a Comment