Thursday, July 4, 2013

TUMECHUKUA NCHI KUTATUA MATATIZO YA KISIASA MISRI

Amiri jeshi mkuu wa Jeshi la Egypt Abdel Fattah al-Sisi amesema kuwa wamefikia maamuzi hayo jana ya kuchukuwa Nchi na kuitawala kutoka katika uongozi wa Rais Mohamed Morsi .

 
Akiwa katika luninga Live Amiri jeshi alitangaza na kusema kuwa Mkuu wa Mahakama ya Katiba ataapishwa kwa lengo la kusimamia shughuli za kiserikali na kuunda serikali kwa lengo la kufanya uchaguzi mapema iwezekanavyo.

Al-Sisi alisema wameamua kufanya maamuzi hayo baada ya Morsi kukataa amri ya Jeshi iliyomtaka kufikia makubaliano na wapinzani hao wa Egypt.

0 comments:

Post a Comment