12:34 AM
SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Siku
ya leo kila utakalolifanya litapuuzwa na watu na kukufanya ukate
tamaa. Hiyo inatokana na nyota yako wikii hii kuingia ukungu.
Jitahidi kuoga na maji ya kisima kuondoa giza katika nyota na mambo
yatafunguka tena.
MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Siku
ya leo kuna habari za kusikitisha utakazozipata hivi , habari hizo
zitakuwa zinahusiana na mambo ya kisheria. Kama una kesi au jamaa
yako ana kesi kuna hatari ya kufungwa. Kuwa muangalifu
MIZANI
– LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Siku ya leo mambo yako mengi
yataharibika,unashauriwa kutopanga mipango yoyote ya pesa kwani
hakuna manufaa yoyote utakayoyapata kwa mchana huu.
NGE -
SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo na kesho mambo uliyoyapanga
hayatatimia, kila utakalolipanga litakwama, unashauriwa kuwa mtulivu
na hali hiyo.Uvumilivu ndio utakusaidia katika kupata mafanikio.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Wiki hii utajikuta
ukiwa na ujasiri wa ajabu katika kukabiliana na mataizo sugu
yanayokusumbua. fanya mambo yako bila kuogopa, hali hii ambayo
itakuongezea kipatao chako.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN
20)
Siku ya leo habari za kimapenzi zitakuwa nyingi, utakutana na
mpenzi wako wa zamani na mtajikuta mkikimbushiana ya zamani.wapenzi
wapya wako njiani na watakuchangana kwani utashindwa umchague yupi.
Tuliza akili na fanya maamuzi ya busara.
NDOO –AQUARIUS (JAN
21 – FEBR 19)
Wiki hii mambo yako yataingiliwa na watu
watakukufanyia khiyana au kukuharibia kazi zako. Unashauriwa kutokata
tamaa na hali hiyo baadaye mambo yatafunguka
SAMAKI – PISCES
(FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo msaada uliokuwa unautegeme kuupata
hautaupata tena, anayetaka kukusaidia ametiwa na maneno na mtu ambaye
unamwamini na ameghairi, jaribu kukutana naye urekebishe
mambo.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Mchana huu katika
matembezi yako ukakuta wendawazimu wawili kwa pamoja Hiyo ni dalili
ya kwamba mambo yako yote yatakwama pia kuna habari za msiba
utazipata katika siku za hivi karibuni.
NG’OMBE – TAURUS
(APR21 – MAY 20)
Siku ya leo mambo yako hayatakuwa mazuri bila
ya kuwashirikisha watu wengi ndiyo yafanikiwe vinginevyo ni mikwamo
tu. Pendelea kufanya kuwatembelea ndugu zako hasa wa kiume.
MAPACHA
- GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Siku ya leo usiende safari uliyoipanga,
kung’ang’ania safari hiyo ni kujitafutia balaa. Unatakiwa kupanga
upya safari hiyo na mambo yako yote kwa ujumla.
KAA –
CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Wiki hii mipango yote ya pesa itakwama
na kama ulikuwa unakwenda kudai pesa unashauriwa kurudi nyumbani
kwani huko uendako hakuna la maana utakalolipata.
0 comments:
Post a Comment