Tuesday, July 30, 2013

BAADA YA TAIFA STARS KUPOTEZA NAFASI YA KUSHIRIKI FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA KOCHA WA TAIFA STARS AFUNGUKA JUU YA TIMU HIYO.


Kocha wa Taifa Stars Kim Paulsen amefunguka na kusema ya moyoni mwake liicha ya kikosi chake kupoteza nafasi ya kushiriki katika fainali za mwakani za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil na Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za ndani (CHAN) zitakazochezwa Afrika Kusini. Kim Poulsen amesema kuwa bado ana imani kubwa na kikosi chake na hivyo hafikirii kukipangua wala kukivuruga kwani kitendo cha kushindwa na wapinzani wao kulitokana na makosa ya Kiufundi na si Uwezo wa wachezaji au kikosi chake hicho.

Kikosi cha Taifa Stars bado kinajengwa na kinaendelea kukuwa siku hadi siku hivyo kinahitaji muda wa kutosha kwa waxchezaji kuwa pamoja na kufanya kazi pamoja ingawa matarajio yake ilikuwa ni kushinda mechi dhidi ya Uganda .

"Ninaiamini timu yangu, bado ni timu nzuri... kufungwa kwetu ni moja ya makosa ya kimchezo na hivyo siwezi kuwalaumu sana wachezaji. Hakikuwa kikosi kibaya," alisema Kim ambaye awali alikuja nchini na kupewa kibarua cha kufundisha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) kabla ya kupandishwa baadaye kufuatia kuondoshwa kwa mtangulizi wake, raia mwenzake wa Denmark, Jan Poulsen.



0 comments:

Post a Comment