Friday, July 5, 2013

NYOTA YAKO LEO IJUMAA: 5/7/2013.


KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Leo kuna kila dalili ya kupata ukitakacho hasa ukikutana na mwanamke mwenye mimba amekaa kibarazani, unashauriwa kuwa mwangalifu katika matumizi yako, kwani kuna hali ya kukwama huko mbele.


SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Dhamira yako ya kuingia katika siasa itapata misukosuko kuna njama unaundiwa za kukukomoa katika maandalizi yako kujiingiza. Ikitokea bahati Leo hii ukatembelewa na Polisi ambaye si rafiki yako basi ujue mipango hiyo itaingia dosari, iahirishe.

MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Leo Kwamba utapata zawadi kubwa kwa kuwa utafaulu katika mitihani utakayoifanya hivi karibuni. Safari yako ipo na huko uendako utapata faida kubwa. Mipango yako iwe ya siri.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Leo ni siku ambayo utakutana na mikwaruzano ya hapa na pale na itatokea itatokea kazini kwako au nyumbani kwako.Unashauriwa usifiche matatizo yako yaelezee ili upate msaada wa kukuondolea matatizo hayo.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Yule mgeni uliyekuwa unamtegemea kuja hivi karibuni, atakuja na habari za kukufurahisha hasa kulingana na masuala ya maisha. Jaribu kumdadisi atakueleza mengi ya kukusaidia.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 23)
Leo hii ukimkuta mtu anasoma kitabu kilichoandikwa katika lugha ambayo huifahamu, hiyo ni dalili ya kupata homa hasa nyakati za jioni, unashauriwa kufanya mazoezi kwa bidii nyakati hizo.


MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo hii ukikutana na Paka na akawa anakufuata bila kufanya fujo, hiyo ni dalili kwamba utakosa fedha leo au utapata hasara ambayo hukuitegemea.Rafiki yako.hatokusamehe madhambi uliyomfanyia

NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 39)
Leo hii ukikutana na mtu ana Sharubu ndefu na zenye kutisha au zisizopendeza, hiyo ni dalili ya kwamba utakumbana na matatizo, vikwazo na ugumu wa mambo yako kwa Leo hii, kuna dalili za kualikwa katika ulevi au wewe kukataa jambo utakaloambiwa na rafiki yako.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo hii unatakiwa ujisahihisha kwa madhambi uliyomfanyia rafiki yako. Akikujia yeye kutaka kujua sababu ya wewe kufanya hivyo mpokee, asipokuja mfuate. Usione taabu kuomba radhi sababu mambo yako yatafunguka.

PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Wiki hii ni nzuri na utagundua siri nyingi ambazo hapo kabla ulikuwa hujazijua. Tegemea kupata mwaliko wa kongamano katika siku mbili zijazo. Na ikitoke ukakutana na mtu kafungwa Pingu, Hiyo ni dalili ya kwamba huko uendako

NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Leo hii ukiwaona Polisi zaidi ya wawili wanatembea pamoja tegemea kupata habari za kesi au kukamatwa kwa mtu unaemtegeme sana katika shughuli zako. Unashauriwa usitembee ikifikia muda wa jioni.

MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Leo hii ukikujia mtu na akataka akuuzie kitu ambacho wewe huna, basi ujue hiyo ni dalili ya kuwa siri zako za nyumba ya nje uliyonayo zimejulikana na mkeo na unatakiwa kuwa mwangalifu umewekewa mtego


0 comments:

Post a Comment