Wednesday, July 10, 2013

NAELEKEA KUWAUNGA MKONO WANANCHI WANGU,KAMA KUPIGWA TUPIGWE WOTE-MAKAMBA

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mh January Makamba amesema yupo teyari kuungana na Wananchi wa Jimbo lake katika madai yao ya kumkataa mwekezaji wa kiwanda cha chai baada ya jeshi la Polisi kutumia Nguvu kubwa kwa kuwapiga na kuwajerui baadhi ya Wananchi hao ambao inasemekana walikuwa tulivu wakiendelea na shughuli zao.

Jana Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto waliamuru kiwanda kifunguliwe hata kwa mtutu wa bunduki na leo wakapelekwa askari polisi wakiwa na silaha. Katika kulazimisha kiwanda kifunguliwe wananchi wamepigwa na watu watano wamejeruhiwa. Kabla ya polisi kwenda hakukuwa na ghasia yoyote, watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Kitendo cha kupigwa wananchi kimewaudhi sana wananchi na kimeniudhi sana na mimi, wanauliza kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki pahala ambapo hapakuwa na fujo na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hiki kumlinda mwekezaji ambaye wananchi kwa kauli moja walimkataa - tena walimkataa kwa amani bila fujo.”

Alimalizia kwa kusema kuwa nimeongea na IGP kwamba kuwe na restraint. Watu wetu huwa sio watu wa fujo. Hata hivyo, watu wakiwa na hisia kwamba wanaonewa wanaweza kufanya chochote. Naelekea huku kuungana na wananchi wangu, kama ni kupigwa tupigwe sote.

Ikumbukwe kuwa Tarehe 26 Mei 2013, wakulima wa Chai Bumbuli waliazimia kumkataa mwekezaji/mbia kwenye kiwanda chao cha Chai Mponde ambaye wanaamini alikuwa anawadhulumu. Pia waliazimia kwamba viongozi wao wa wakulima wa Chai ambao wameshindwa kusimamia maslahi yao na kujali matumbo yao tu, waondoke. Vilevile, waliamua kuuza chai yao kwenye viwanda vya jirani na hivyo kiwanda cha Mponde kufungwa. Na katika kipindi chote hiki kumekuwa na utulivu wananchi wakisubiri suluhu ya matatizo yao.

0 comments:

Post a Comment