Mwenyekiti
wa (Chadema) ambae pia ni diwani wa Wilaya ya.......
Rorya, mkoani
Mara katika kata ya Tai, Masirori Kyorang, amepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Mwanzo Shirati, akikabiliwa na kesi ya kushikwa
ugoni na mke wa mlinzi wa Mbunge wa Jimbo la Rorya.
Masirori
alikamatwa Julai 24 kwaka huu katika nyumba ya kulala wageni ya Tripo
Kabwana akiwa na mwanamke huyo Pendo Omolo.
Mume
wa mwanamke huyo ambaye ni mmoja ya walinzi wa Mbunge wa Jimbo la
Rorya katika majengo yake wilayani humo, Ochieng Ninja alipata
taarifa ya kuonekana mke wake ndani ya nyumba ya kulala wageni akiwa
na Mwenyekiti huyo wa Chadema Wilaya ya Rorya.
mlinzi
huyo baada ya kufika katika nyumba hiyo ya wageni aliomba msaada wa
watu ambao walijitokeza na kuwakamata mtuhumiwa na mwanamke huyo.
0 comments:
Post a Comment