Ni wazi kabisa
kwamba Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ,ni
kitovu cha kusafirisha dawa za kulevya nje ya nchi,kwani kumekuwa na
urahisi na wepesi wa watu hao kupita kwa kuwa tu wanaofanya biashara
hiyo ni watu wasiokamatika wala kuzuiliwa ndio maana inaendelea
kushamili na kukuwa kila siku.
takribani wiki mbili
tu, Watanzania wanne wamekamatwa ughaibuni wakiwa na shehena ya dawa
hizo ambazo walisafirisha kutoa Tanzania kwenda nje kupitia uwanja
huo bila ya kukamatwa.
Mara ya kwanza walikuwa
ni wasichana wawili, Agnes Jerald (25) na Melisa Edward (24), ambao
walikamatwa Afrika Kusini na kushtakiwa nchini humo.
Kamanda wa Polisi
Kikosi cha Viwanja vya Ndege Nchini, Deusdedit Kato, alisema jalada
la upelelezi kuhusu tukio la kukamatwa kwa wasichana Afrika Kusini
litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) leo ingawa hakuwa tayari
kutaja watuhumiwa ni nani hasa wanaoshirikiana na wafanyabiashara ya
dawa
“Siwezi kukuambia ni
nini kimepatikana katika uchunguzi wala kutaja majina ya watu, kwa
kuwa mimi ninapeleka nilichokichunguza kwa sababu naweza kukuambia
lakini ikawa sio hivyo kwani huu ni uchunguzi tu,” alisema.
Aliongeza: “Naweza
kupeleka jalada langu la uchunguzi kwa DDP lakini kutokana na utalaam
wake akagundua kuna mapungufu, hapo tayari nitakuwa nimepotosha umma.
Lakini pia akiona upelelezi unajitosheleza yeye ndiye anaweza kuamua
kupeleka Mahakamani.”
Nae Waziri wa
Uchunguzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye amejipatia sifa za utendaji
katika siku za hivi karibuni, kwa kuendesha timua timua katika
taasisi zinazosimamiwa na wizara yake kwa tuhuma za uzembe, amekuwa
kimya na pengine kukwepa kabisa kutia mguu katika sakata la dawa za
kulevya JNIA.
Wiki iliyopita Dk.
Mwakyembe mwenye dhamana ya Viwanja vya Ndege nchini tulitaka kujua
ni hatua gani amechukua, lakini alijibu kwamba hana taarifa za kina
kuhusu sakata hilo.
sakata hilo la Madawa
ya Kulevya limempa kigugumizi Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, ambaye hakutaka kuzungumzia
sakata hilo na kusema liko kwa Kamanda wa Polisi, Kitengo cha Kuzuia
na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzowa.
ila sasa Kamanda Nzowa
alipoulizwa alisema upelelezi bado unaendaelea kubaini mambo
mbalimbali yaliyoko nyuma ya tukio hilo. Alipoulizwa ikiwa Polisi
wamebaini mmiliki pamoja na maofisa walioruhusu kupitishwa kwa dawa,
Nzowa alisema uchunguzi unaangalia mambo mengi na ndiyo huo utakuja
na taarifa kamili.
0 comments:
Post a Comment