Friday, July 19, 2013

HIVI NDIVYO MNYIKA ALIVYOMTENDA JANUARY MAKAMBA LEO

Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano Tanzania January Makamba amelalamikia kitendo cha Mbunge wa Ubungo Mh John Mnyika baada ya kuiuweka namba yake katika mitandao na kutaka watu wampigie na kumtumia sms ili watoe maoni yao juu ya Kodi ya simu ilikwisha anza kazi toka mwanzoni mwa mwezi huu.
kaweka namba yangu ya simu ya mkononi ili watu wanipigie na kutukana. Nadhani ni siasa isiyo ya kistaarabu. Hadi sasa nimepata messages zaidi ya 600. Sio sahihi kabisa. “
Aliendelea kufafanua Kuwa Wabunge WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini.



Makamba aliongeza kuwa Namheshimu Zitto Kabwe kwasababu alitoa kauli immediately ya kusema anaona aibu kuwa sehemu ya Bunge hili na kwamba wawakilishi wa wananchi wamewaangusha wananchi. Mwenzake John Mnyika anajitoa fahamu na kufanya harakati kupitia press releases.

Suluhisho hapa sio kulumbana wala kutupiana lawama. Suluhisho ni kurudi Bungeni na kubadilisha pale tulipokosea. Sio kutafuta umaarufu mitandaoni. Kunapotokea kosa, tunasahihisha haraka then we move on.


0 comments:

Post a Comment