Madiwani
wanane wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kati ya
madiwani 28 wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, wamesusia mkutano
wa hadhara wa Waziri Mkuu wa Mizengo, Mizengo Pinda, uliofanyika.......
kwenye viwanja vya manispaa hiyo kwa madai ya kusimikwa bendera ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano huo.
Tukio
hilo lilitokea Jumamosi kati ya saa 8:30 mchana na 9:00 alasiri
wakati madiwani wa halmashauri hiyo wakijiandaa kwenda kwenye mkutano
huo wakiwa tayari wamevaa majoha.
Hata
hivyo, madiwani wanane wa Chadema, waliamua kuvua majoho hayo na
kuondoka kwenye eneo la Manispaa huku wakidai kuwa katika eneo la
mkutano kuna bendera ya CCM kinyume cha utaratibu.
Kwa
msingi huo, madiwani wanane wa Chadema walikataa kuudhuria mkutano
huo.
Chanzo
Nipashe







0 comments:
Post a Comment