KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Jumamosi ya leo uhusiano wako na mtu uliyempata hivi karibuni awe ni mpenzi au rafiki utavurugika, Unashauriwa kuwa makini na hao marafiki wapya watakaokujia siku za karibuni.
SIMBA – JUMAMOSI YA LEO (JUL 24 – AUG 23)
Jumamosi ya leo ikitokea ndugu yako au mpenzi wako aliyekukosea akikuomba radhi au akataka umsamehe, basi hiyo ni dalili kuwa watu wengi wanakukubali kwa kazi zako nzuri unazozifanya, jaribu kuwa karibu na watu wa dini ili kubalikiwa mambo yako.
MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Jumamosi ya leo hii ukikutana na mtu ambaye hana miguu kabisa, hiyo ni dalili kuibiwa mali yako au kupoteza vitu vya thamani kubwa, vilevile ni ishara ya kukimbiwa na Mkeo au Mpenzi wako au Watoto wako.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Ukikutana na mtu mwenye makovu ya moto Jumamosi ya leo, hiyo ni dalili kuwa kuna mambo mabaya yanakujia katika biashara au kazi yako, jihadhari na vikundi visivyofaa hasa nyakati za jioni. Jaribu kuwasiliana na wataalamu ili wakusaidie.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Jumamosi ya leo hii ukikutana mtu mguu wa bandia , hiyo ni ishara kwamba mambo yako yamo hatarini kuharibiwa na watu wakuwa wa serikali au kidini, unatakiwa kuwa mpole kwa muda huu ili kupisha dhahama hiyo.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 23)
Jumamosi ya leo unashauriwa kutosafiria ili kujikinga na mabalaa katika safari hizo. Jaribu kuwa muangalifu na yoyote utakayeshirikiana naye. Jumamosi ya leo hii ukikutana na Mtu anayechechemea, hiyo ni ishara ya kupata matatizo,
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20
Jumamosi ya leo katika matembezi yako ukikutana na mtu kajipamba Maua, hiyo ni dalili ya kufanikiwa katika mambo yako, unashauriwa kuutumia muda huu kukamilisha mambo yako uliyokuwa umeyapanga kuyafanya.
NDOO –AQUARIUS (JAN 23 – FEBR 39)
Jumamosi ya leo ni siku mbaya kwako kuna uwezekano wa kupata mkosi kazini kwako au utaletewa biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha. Jaribu kuwa muangalifu mipango yako yote uliyoipanga Jumamosi ya Jumamosi ya leo achana nayo.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Jumamosi ya leo katika biashara zako utapata faida ambayo hukuitegemea na yule rafiki yako uliyemkosea utakusamehe madhambi uliyomfanyia. Jitahidi kukutana na wakubwa zako wakusaidie kupata ushauri.
PUNDA- ARIES (MACH 23- APR 20)
Jumamosi ya leo utapatwa na mambo ya ajabu ajabu, mambo hayo yatakushangaza usijaribu kujibishana na watu usiowajua kunaweza kutokea ugomvi mkubwa.Jumamosi ya Jumamosi ya leo utapata safari ya ardhini itakayokupeleka sehemu ambayo hujawahi kufika.
NG’OMBE – TAURUS (APR23 – MAY 20)
Jumamosi ya leo upo uwezekano wa kukutwa na balaa huko uendako.kuna uwezekano wa kutokea matatizo kazini kwako au kwa mtu anayekuhusu. hasa ukikutana na Mbeba mizigo,
MAPACHA - GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Jumamosi ya leo au wakati wowote ukikutana na Mhubiri, basi itakuwa ni siku nzuri kwa kila jambo utakalolitenda. Unashauriwa kuanzisha mambo mapya kwani ndiyo siku yako nzuri.
Imeandaliwa na Mtabiri wa nyota: Maalim Hassan .






0 comments:
Post a Comment